User:Abdi M. Abdallah

From Wikimania 2010 • Gdańsk, Poland • July 9-11, 2010

Maandishi ya kichwa

CHAWAKAMA

CHAWAKAMA ni akronimu ya Chama Cha Kiswahili cha Wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya afrika Mashariki. Chama hiki kiliasisiwa Novemba, 2004 Dar-es-salam nchini Tanzania. Vyuo vilivyoshiriki katika kuanzisha Chama hiki ni: Chuo Kikuu cha Moi(Kenya), Chuo Kikuu cha Makerere(Uganda) na Chuo Kikuu cha Dar-es-salam(Tanzania).

CHAWAKAMA kimeandaa makongamano kadha ya kuwahamasisha Wanafunzi wa Vyuo Vikuu kuhusu lugha ya Kiswahili. Kwamba Kiswahili ni lugha ya Afrika ambayo inaweza kutuunganisha pamoja kama Waafrika. Pia lugha hii ni lugha ya mawasiliano, maendeleo ya uchumi na pia itatumika kudumisha tamaduni zetu za Kiafrika hapa Bara Afrika.

Chama hiki kimeenea kote Afrika Mashariki. Kongamano la CHAWAKAMA mwaka 2009 uliandaliwa nchini Kenya katika Chuo Kikuu Cha Nairobi- Bewa la Kikuyu. Ikateuliwa kuwa kongamano la sita la CHAWAKAMA mwaka 2010 litaelekea nchini Uganda mjini Mbarara. Kongamano hilo lilifana sana na viongozi wapya wakachaguliwa. Nao ni kama wafuatao:

  1. Mwenyekiti- Bw. Abdi M. Abdallah (Chuo Kikuu cha Kenyatta- Kenya)
  2. Makamu Mwenyekiti- Bw. Ntakirutimana Jean Pascal (Universite Du Burundi- Burundi)
  3. Katibu Mkuu- Bw. Said Taqwir Mukisa (Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro- Tanzania)
  4. Naibu Katibu- Bw.Muthahinga Moses (Chuo Kikuu cha Askofu Stuart- Uganda)
  5. Mhazini- Bw. Harerimana Jean claude (Chuo Kikuu cha Elimu Kigali{KIE}- Rwanda)
  6. Naibu Mhazini- Bw. Niyonkuru Isaac (Universite Du Burundi- Burundi)
  7. Mhariri Mkuu- Bw. Paul A. Sheka (Chuo Kikuu cha Arusha- Tanzania)
  8. Naibu Mhariri- Bi. Akola Josephine Sabatia (Chuo Kikuu cha masinde Muliro- Kenya)

Afisa wa Uhusiano bora alitoka nchi ya Uganda.

Baada ya kongamano hili, iliamuliwa kuwa kongamano la saba la CHAWAKAMA litaandaliwa nchi ya Burundi kule jijini Bujumbura.

Kauli mbiu ya CHAWAKAMA ni: "KISWAHILI HAZINA YA AFRIKA KWA MAENDELEO ENDELEVU"

- Abdi M. Abdallah 14:38, 29 November 2010 (UTC)